Saturday, August 31, 2013

KUTAMBUA FURSA ZA BIASHARA

Fursa ni mapengo ya mahitaji yaliyoko katika jamii yanayohitaji         kuzibwa.   Kwa maana ingine fursa ni hitaji, nafasi au changamoto au mazingira fulani ambayo mjasiriamali hutumia kuibua wazo la biashara. Wazo la biashara ndio chimbuko la biashara.

Mjasiriamali ana mazingira yanayomsaidia kutambua fursa ya biashara.
a)      Mazingira ya ndani/Maisha binafsi
-     Mjasiriamali anapaswa kuangilia maisha yake binafsi.
-        Kazi alizowahi kufanya huko nyuma
-        Mambo unayoyapenda kufanya mara kwa mara
b)      Mazingira  ya nje
-        Watu wanaokuzunguka
-        Maeneo unayopenda kutembelea mara kwa mara
-        Mahitaji ya jamii unayoyaona

Njia zifuatazo humsaidia mtu kutambua fursa ya biashara
1.      Vyombo vya habari kama magazeti, redio, TV.
2.      Mitandao ya Komputa yaani Inteneti
3.      Majarida
4.      Maonesho ya biashara
5.      Machapisho ya magari
6.      Mazungumzo
7.      Kusafiri sehemu moja hadi ingine
8.      Mihadhara
9.      Kufuatilia sera ya nchi mfano kilimo kwanza
10.   Kutembelea taasisi za biashara
11.   Watoa ushauri kuhusu biashara

Fursa sawa kwa wote, chukua hatua.








Friday, August 30, 2013

MAFUNZO YA TASEA 2013

TASEA kwa 2013 iliendesha mafunzo ya ujasiriamali katika Lodge ya Stella Maris iliyopo Mailisita Hai Kilimanjaro. 

Zifuatazo ni baadhi ya picha wakati wa Mafunzo. 

                       Afisa ustawi wa jamii kutoka Mkombozi Center  akifuatilia mafunzo.

                                Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza mwezeshaji (hayuko pichani) 

MIFANO YA BIASHARA UNAZOWEZA KUANZISHA ( kwa wafanyabiashara wadogo)

Kila mtu ana uwezo wa kuanzisha biashara ya kwake tofauti na mtu mwingine. Ifuatayo ni mifano michache ya biashara ambayo mtu anaweza kuanzisha na kujiongezea kipato.

A. WAFANYABIASHARA WA REJAREJA

1.    Vibanda vya bidhaa
2.    Wachuuzi wa matunda na mboga
3.    Wauza mitumba
4.    Maduka ya samani
5.    Vituo vya mafuta
6.    Maduka ya vyakula
7.    Duka la matunda na mboga
8.     Duka la nguo na viatu
9.    vifaa vya nyumbani na shamba  
10. Duka la vifaa vya umeme
11. Maduka ya mashine za shamba
12. Duka la vifaa vya kuandikia
13. Duka la madawa
14. Duka la kuoka mikate
15. Duka la bidhaa mchanganyiko
16. Duka la sare za shule
17. Duka la nyama


B. WAZALISHAJI NA WAKULIMA WADOGOWADOGO



1.   Mpakiaji bia katika chupa
2.   Mpakiaji soda katika chupa
3.   Watengenezaji wa samani na mbao
4.   Wayeyushaji wa chuma
5.   Mafundi cherehani
6.   Kazi za mikono( vikapu, mitingu, vyungu)
7.   Wafumaji
8.   Wasuka mikeka
9.   Watengeneza matofali