Tuesday, September 24, 2013

DHANA YA UJASIRIAMALI



MAANA YA UJASIRIAMALI



Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwa hizo ni; Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.

Pia katika hali nyingine Mjasiriamali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha mwenyewe(amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara.

Neno Ujasiriamali lina asili ya Kifaransa " Entreprendre" sawa na Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara katika maana rahisi ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri.

Kwa mitazamo mbalimbali ya wasomi wana muelezea Mjasiriamali kama mtu ANAYEONGOZA, ANAYEPANGA na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/shughuli yake husika.  Vilevile ni mtu anayechukua hatua pindi fursa itokeapo.

Mchumi wa KiAustrian Joseph Schumpeter ameielezea dhana ya ujasiriamali kwa kuegemea mihimili ya UGUNDUZI na UBUNIFU, katika nyanja hizi(yaani kugundua na kubuni):-
  • Bidhaa Mpya
  • Njia Mpya za uzalishaji/uendeshaji.
  • Masoko Mapya
  • Mifumo mipya ya Vikundi na Mashirikisho

UTAJIRI unapatikana pindi UGUNDUZI unapoenda sambamba na MAHITAJI, kwa mtazamo huu tunaweza kusema ya kwamba kazi ya Mjasiriamali ni sawa na kuunganisha mbegu za vigezo fulani katika hali ya Ugunduzi na Ubunifu ili kutengeneza ubora na thamani kwa mteja kwa imani ya kwamba thamani itakayopatikana itafidia gharama za mbegu hizo, na hatimaye kutengeneza faida ya kutosha inayopelekea UTAJIRI.

Mpaka hapa tumeweza kumfahamu huyu Mjasiriamali kwa maana na Mitazamo michache. Je kila Mfanya biashara ndogo ndogo ni Mjasiriamali? Tathmini hili kabla hujasoma Article nyingine!

Historia ya ujasiriamali Tanzania

Tuesday, September 10, 2013

UPS AND DOWNS OF THE ENTREPRENEURS IN THE WORLD




I hope this information will motivate you and provide you with courage when you experience ups and downs in your career, business or entrepreneurship initiatives in particular. Not everyone who’s on top today got there with success after success. More often than not, those who history best remembers were faced with numerous obstacles that forced them to work harder and show more determination than others. Next time you’re feeling down about your failures in college or in a career, keep these fifty famous people in mind and remind yourself that sometimes failure is just the first step towards success. Business Gurus These businessmen and the companies they founded are today known around the world, but as these stories show, their beginnings weren’t always smooth.

 1. R. H. Macy: 

Most people are familiar with this large department storechain, but Macy didn’t always have it easy. Macy started seven failedbusiness before finally hitting big with his store in New York City.

2. F. W. Woolworth:
Some may not know this name today, but Woolworth was once one of the biggest names in department stores in the U.S. Before starting his own business, young Woolworth worked at a dry goods store and was not allowed to wait on customers because his boss said he lacked the sense needed to do so.

3. Soichiro Honda:
 

 The billion-dollar business that is Honda began with a series of failures and fortunate turns of luck. Honda was turned down by Toyota Motor Corporation for a job after interviewing for a job as an engineer, leaving him jobless for quite some time. He started making scooters of his own at home, and spurred on by his neighbors, finally started his own business.

4. Akio Morita:
 

 You may not have heard of Morita but you’ve undoubtedly heard of his company, Sony. Sony’s first product was a rice cooker that unfortunately didn’t cook rice so much as burn it, selling less than 100units. This first setback didn’t stop Morita and his partners as they pushed forward to create a multi-billion dollar company.

5.  Bill Gates: Gates didn’t seem like a shoe-in for success after dropping out of Harvard and starting a failed first business with Microsoft co-founder Paul Allen called Traf-O-Data. While this early idea didn’t work, Gates’ later work did, creating the global empire that is Microsoft.


Wednesday, September 4, 2013

MCHAKATO WA KUANZISHA BIASHARA

Biashara ni sawa na taasisi zingine, katika uanzishwaji wake kuna mchakato muhimu wa kufuata. Ebu zingatia hatua hizi hapa chini kama una mpango wa kuanzisha biashara yako. 

1. Kupata wazo la biashara 

 - Wazo la biashara ni maelezo mafupi juu ya shughuli ya uzalishaji mali anayotaka kufanya     mjasiriamali. 
 - Mjasiriamali anapaswa kufikiri juu ya biashara ya aina gani ana anaweza kufanya katika eneo husika. Je ana ujuzi au uzoefu gani juu biashara anayotaka kufanya? Rasilimali gani anatakiwa kuwa nazo ilikutekeleza wazo lake.
 - Je anafahamu kwa kiasi gani soko la biashara anayotaka kufanya.
 - Je atawapata wataalam wa kumsaidia katika kufanikisha wazo lake ? 
- Mtaji kiasi gani unahitajika ? 

2. Kujenga hoja:

  Baada ya tathimini hapo juu mjasiriamali anapaswa kujenga hoja kama ifuatavyo 
- Kuunda biashara kichwani
 - Aweke wazo lake katika maandishi 
- Atajiuliza zaidi maswali ya msingi juu ya bidhaa au huduma anazotaka kufanyia kazi. 
-Uhakika wa soko ukoje, mtaji utapatikanaje, atauzaje bidhaa au huduma, sehemu ya biashara itakuwa wapi ? washindani wngapi ? ulinzi na usalama katika eneo husika ukoje ? taratibu za kisheria zikoje ? Muda gani utahitajika kufanya maandalizi ? kuweka malengo. 

Sunday, September 1, 2013

SALAMU ZA JUMAPILI

TASEA inawatakia wasomaji wake jumapili njema.  Ni siku muhimu sana katika maisha, siku ya kumkumbuka muumba ni siku ya kuheshimiwa. Ni siku ambayo familia kula na kunywa pamoja, kusali pamoja. Katika yote furaha ipewe  kipaumbele. 

TASEA family  iko pamoja nanyi katika yote mema.

EXPERIENCE FINANCIAL FREEDOM