MAANA YA UJASIRIAMALI
Dhana ya Ujasiriamali
ina maana pana , miongoni mwa hizo ni; Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa
kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia
za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri)
ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.
Pia katika hali
nyingine Mjasiriamali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha
mwenyewe(amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara.
Neno Ujasiriamali lina
asili ya Kifaransa " Entreprendre" sawa na
Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara katika
maana rahisi ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri.
Kwa mitazamo
mbalimbali ya wasomi wana muelezea Mjasiriamali kama mtu ANAYEONGOZA,
ANAYEPANGA na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza
katika biashara/shughuli yake husika. Vilevile ni mtu anayechukua hatua pindi fursa
itokeapo.
Mchumi wa KiAustrian
Joseph Schumpeter ameielezea dhana ya ujasiriamali kwa kuegemea mihimili ya
UGUNDUZI na UBUNIFU, katika nyanja hizi(yaani kugundua na kubuni):-
- Bidhaa Mpya
- Njia Mpya za uzalishaji/uendeshaji.
- Masoko Mapya
- Mifumo mipya ya Vikundi na Mashirikisho
UTAJIRI unapatikana pindi UGUNDUZI unapoenda sambamba
na MAHITAJI, kwa mtazamo huu tunaweza kusema ya kwamba kazi ya Mjasiriamali ni
sawa na kuunganisha mbegu za vigezo fulani katika hali ya Ugunduzi na Ubunifu
ili kutengeneza ubora na thamani kwa mteja kwa imani ya kwamba thamani
itakayopatikana itafidia gharama za mbegu hizo, na hatimaye kutengeneza faida
ya kutosha inayopelekea UTAJIRI.
Mpaka hapa tumeweza
kumfahamu huyu Mjasiriamali kwa maana na Mitazamo michache. Je kila Mfanya
biashara ndogo ndogo ni Mjasiriamali? Tathmini hili kabla hujasoma Article
nyingine!
Historia ya
ujasiriamali Tanzania
Kutokana na utandawazi
kuenea duniani, mfumo wa sera ya kibepari ulichukua nafasi kubwa duniani. Mfumo
wa kibepari unasisitiza watu binafsi kumiliki na kuendesha biashara, serikali
jukumu lake ni kupanga sera na kuisimamia.
Mwishoni mwa miaka ya 1980 Tanzania ililazimika kuiga sera ya kibepari
kutokana na masharti ya Benki Kuu ya Dunia
( World Bank) na Shirika la Fedha
Duniani ( IMF).
Ni kipindi cha uongozi
( utawala) wa awamu ya tatu, dhana ya ujasiriamali ilishika kasi sana. Viongozi
wa serikali na wa jamii kwa ujumla walisisitiza watu kujiingiza katika
ujasiriamali kwa maana ya kuanzisha na kuendesha biashara. Serikali kwa
asilimia kubwa ikajiatoa katika uzalishaji. Makampuni binafsi yalishika kasi
kubwa.
SEKTA ZA UCHUMI
Kuna sekta ya umma na sekta binafsi. Kuhusu
sekta ya umma ni kwamba serikali ni mzalishaji na msimamizi, mkazo mkubwa ni
watu kusoma na baada ya kisoma ni kuajiriwa.
Dhana ya sekta binafsi inahusu watu binafsi kumiliki biashara (
Kujiari).
Karne hii lengo la
kusoma shule si kuajiriwa baada ya kumaliza kisoma, lengo kuu ni
kujiajiri. Ni muhimu watu kutafuta
maarifa na ujuzi katika mambo mbalimbali kwa njia mbalimbali mfano semina, internet na vyombo vya habari n.k
No comments:
Post a Comment