Biashara ni sawa na taasisi zingine, katika uanzishwaji wake kuna mchakato muhimu wa kufuata. Ebu zingatia hatua hizi hapa chini kama una mpango wa kuanzisha biashara yako.
1. Kupata wazo la biashara
- Wazo la biashara ni maelezo mafupi juu ya shughuli ya uzalishaji mali anayotaka kufanya mjasiriamali.
- Mjasiriamali anapaswa kufikiri juu ya biashara ya aina gani ana anaweza kufanya katika eneo husika. Je ana ujuzi au uzoefu gani juu biashara anayotaka kufanya? Rasilimali gani anatakiwa kuwa nazo ilikutekeleza wazo lake.
- Je anafahamu kwa kiasi gani soko la biashara anayotaka kufanya.
- Je atawapata wataalam wa kumsaidia katika kufanikisha wazo lake ?
- Mtaji kiasi gani unahitajika ?
2. Kujenga hoja:
Baada ya tathimini hapo juu mjasiriamali anapaswa kujenga hoja kama ifuatavyo
- Kuunda biashara kichwani
- Aweke wazo lake katika maandishi
- Atajiuliza zaidi maswali ya msingi juu ya bidhaa au huduma anazotaka kufanyia kazi.
-Uhakika wa soko ukoje, mtaji utapatikanaje, atauzaje bidhaa au huduma, sehemu ya biashara itakuwa wapi ? washindani wngapi ? ulinzi na usalama katika eneo husika ukoje ? taratibu za kisheria zikoje ? Muda gani utahitajika kufanya maandalizi ? kuweka malengo.
3. Kukadiria na kutafuta rasimali
- Eneo la biashara
- Nguvu kazi
- Mtaji
- Taratibu za kisheria
4. Maandalizi ya kuanzisha biashara
- Mjasiriamali anapanga utaratibu wa kitu gani kianze
- Kutafuta leseni ya biashara
- Kuajiri wafanyakazi
5. Kufungua biashara
- Bidhaa tayari ziko dukani au katika eneo husika
- Kuwa na daftari la orodha ya bidhaa na gharama zake.
6. Ufuatiliaji na tathimini
- Kufuatilia kama biashara inaenda kama inavyotakiwa
Tathimini hutoa mwanga kitu gani kifanyike ili biashara itengeneze faida.
No comments:
Post a Comment